Moordeich Mdhamini wa riadha
Asanteni sanaMatokeo ya pili ya wafadhili wa riadha yaliyoandaliwa na wanafunzi kutoka katika shule ya Lise Meitner huko Moordeich Ujerumani yalizidi matarajio yaliyotegemewa:Wanafunzi 367 wa darasa la tano hadi la saba wakike na wakiume walikamilisha kukikimbia riadha jumla ya kilomita 4,381 na hivyo walifanikiwa kupata kiasi cha € 11,979 kwa ajili ya nia njema. Kila mwanafunzi alimtafuta mdhamini ambaye alipaswa kumlipia kiasi kilichokubaliwa kwa kila kilometa 800. Mkimbia riadha mwenye uthubutu zaidi alikimbia mizunguko 24 kiasi cha takribani 19.2 km.
Mwalimu Cornelia Geers alikutana na mradi wa Upendo Daima wakati akiwa mafunzoni katika shule ya jirani mjini Mwanza, jiji la pili kwa ukubwa nchini Tanzania. Shule ambayo watoto wa Upendo Daima wanasomea pia Tuna shukuru sana. Asanteni sana!